Loading...

Mkuu wa mkoa kagera avunja Bodi ya Ushirika kwa tuhuma za ubadhirifu

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum ameivunja Bodi ya Shirika la Maendeleo la kata tatu zilizoko wilayani Misenyi za Ishozi,Ishunju na Gera ili ipishe uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha zilizobainishwa na tume maalumu iliyoundwa na mkuu huyo kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo kati ya baadhi ya wanachama wa shirika hilo na bodi iliyovunjwa.

Tamko la kuivunja bodi hiyo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denis Mwila kwa niaba ya mkuu wa mkoa huyo ambaye ameteua bodi ya muda itakayoongoza shirika hilo kwa kipindi cha miezi 6 ambayo itakuwa chini ya mwenyekiti Kamala Mpaya ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea na amewaagiza wajumbe wa bodi iliyovunjwa kukabidhi mali zote kwa bodi mpya,pia akaahidi kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wajumbe wa bodi iliyovunjwa watakaoangukiwa na tuhuma baada ya uchunguzi kukamilika.

Kwa upande wake,Mrajisi Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkoa wa Kagera Charles Mwafimbo ameeleza baadhi sababu zilizopelekea kuvunjwa kwa bodi hiyo kuwa ni pamoja matumizi mabaya ya fedha zaidi ya shilingi milioni 41 zilizotolewa shirika Hedemora kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ya shule ya sekondari ya Tweyambe ambazo hazijulikani zilipo,kuuza msitu wa shirika hilo na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya mpya iliyoteuliwa Kamala Mpaya amesema kwa sasa hawezi kusema mengi kwa kuwa ni mapema muno ila ameahidi kufanya kazi kwa kutanguliza mbele maslahi ya wanachama wa shirika hilo,naye William Rutta diwani wa kata ya Ishozi amepongeza uamzi uliochukuliwa wa kuivunja bodi ya zamani kwa kusema utailifufua shirika hilo.

Source: ITV
Mkuu wa mkoa kagera avunja Bodi ya Ushirika kwa tuhuma za ubadhirifu Mkuu wa mkoa kagera avunja Bodi ya Ushirika kwa tuhuma za ubadhirifu Reviewed by Zero Degree on 3/12/2017 09:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.