Loading...

Kuelekea mechi ya kesho, Mourinho adai haoni jipya katika mfumo unaotumiwa na Chelsea chini ya Conte

Homa ya pambano kati ya Chelsea dhidi ya Manchester United inazidi kupanda. Usiku wa Jumatatu Manchestet United bila mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovich,watasafiri hadi Stamford Bridge kuwavaa Chelsea.

Chelsea ambao wanaonekana hatari sana msimu huu chini ya Muitaliano Antonio Conte wataingia dhidi ya United bila majeruhi.

Kocha wa Man United Jose Mourinho ameanza kuwashambulia Chelsea kabla hata ya pambano hilo. Mourinho amekuwa akizungumzia sana aina ya uchezaji wa Chelsea msimu huu na amelisema tena. 

Ni kama Mourinho anaona Chelsea hawana jipya kwani anasema anaona bado wanacheza kukaba zaidi, style ambayo wakati yeye yupo klabuni hapo alikuwa akishambuliwa sana kwamba ni mkabaji zaidi.

Mourinho anashangazwa na wanaofurahia aina ya uchezaji wa Chelsea chini ya Conte. Akiongea na shirika la utangazaji Uingereza Bbc alisema “Ninashangazwa na jinsi wanavyocheza, nilidhani labda walimleta (Conte) kujaribu kutafuta aina mpya ya uchezaji ila bado Chelsea ni klabu bora katika ukabaji”.

Msimu huu Chelsea wamekuwa wazuri sana kuzuia huku wakishambulia kwa kuahtukiza(counter attacks). Wakati Jose Mourinho alipokuwa Chelsea alipondwa sana kwa mfumo wake ambao nao ulikuwa kama huu wa Chelsea wa kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza. Mourinho anashangaa Conte kusifiwa kwa kitu ambacho yeye amewahi kupondwa alipokuwa akikifanya.

Mourinho amesema haendi Stamford Bridge kujaribu kulipa kisasi.Lakini wanenda kucheza soka na pia anaenda Stamford Bridge kukutana na baadhi ya marafiki zake. United anakwenda Stamford Bridge na kumbukumbu ya kipigo cha bao 4 kwa 0 walichokipata mara ya mwisho timu hizo zilipopambana.
Kuelekea mechi ya kesho, Mourinho adai haoni jipya katika mfumo unaotumiwa na Chelsea chini ya Conte Kuelekea mechi ya kesho, Mourinho adai haoni jipya katika mfumo unaotumiwa na Chelsea chini ya Conte Reviewed by Zero Degree on 3/12/2017 09:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.