Loading...

Umesikia tambo za Kagera Sugar kwa Simba??

Mecky Maxime
KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema anafahamu ugumu wa mechi na Simba, hivyo amekiandaa kikosi chake kushinda.

Kagera inatarajia kuikaribisha Simba kwenye uwanja wa Kaitaba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii.

Maxime alisema anajua mechi hiyo itakuwa ngumu pengine kuliko mechi zote kutokana na nafasi waliyo nayo Simba katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu.

“Mechi kama hizi huwa ngumu sana maana Simba yupo kwenye nafasi ya kutwaa ubingwa hivyo kwa vyovyote vile atataka kushinda, nasi kwa vyovyote hatutaka kufungwa maana hata sisi tunataka kujiimarisha kumaliza kwenye nne bora,” alisema.

Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 55 na Kagera inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 42 na inayo nafasi ya kupanda zaidi kama itafanya vizuri katika mechi zake zilizosalia.

“Sio kwamba tunaidharau Simba, hapana iko vizuri na wachezaji wake wanabadilika kila siku, ilivyoanza ligi si kama inavyomaliza sasa wameimarika zaidi alisema.
Umesikia tambo za Kagera Sugar kwa Simba?? Umesikia tambo za Kagera Sugar kwa Simba?? Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 12:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.