Loading...

Samsung yaja na simu mpya ya Galaxy S8 iliyofanyiwa maboresho zaidi

Simu mpya zinazotajwa kuwa zimefanyiwa maboresho zaidi zinazinduliwa na kampuni ya Samsung.

Skrini za simu za Galaxy S8 na ya ile iliyo kubwa kidogo ya Galaxy S8+, ni kubwa licha ya kuwa ndogo kuliko zile za mwaka uliopita za S7 na S7 Edge.

Wakati huu simu hizo zote zina skrini zilizojipinda hadi pembeni mwa simu.

Uzinduzi huo unafuatia kufeli kwa simu aina ya Note 7 ambayo ilirushwa mara mbii kufuaiua visa vya kuwaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini ilidai kuwa betri ndiyo ilikuwa na tatizo.

Kampunia hiyo pia imekuwa ikichunguzwa kwa madai kuhusika kwenye ufisadi nchini mwake.

Siku ya Galaxy S8 inatajwa kuwa muhimu zaidi kuwai kuzinduliwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Simu hiyo inatajwa kuwa bora, lakini Samsung itahitaji kujitahidi ziadi ili kuepuka kasoro uliyokumba simu ya Note 7.

Simu hiyo itatolewa rasmi tarehe 21 mwezi Aprili mwaka huu, ambapo Galaxy S8 itauzwa dola 856 nayo S8+ itauzwa dola 968.
Samsung yaja na simu mpya ya Galaxy S8 iliyofanyiwa maboresho zaidi Samsung yaja na simu mpya ya Galaxy S8 iliyofanyiwa maboresho zaidi Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 01:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.