Loading...

Burundi yawataka raia wake waliokimbilia nchi jirani kurejea.

Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika kambi za wakimbizi nchini, wametakiwa kurejea nchini mwao kutokana na kuwepo kwa hali ya amani inayowawezesha wananachi kufanya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kilimo na kuacha kuikimbia nchi hiyo kwa kisingizio cha kuwepo kwa machafuko.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Ruyigi nchini Burundi, moja ya mikoa ya mpakani ambayo wananchi wake wanaendelea kukimbilia nchini, baada ya mkutano wa ujirani mwema kati ya mikoa ya mpakani na wilaya ya Kibondo ambapo amesema nchi hiyo kwa sasa hakuna tatizo la kiusalama huku wananchi wa Burundi wakieleza kuwa wanaoikimbia wanafuata chakula cha bure kambini.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibondo Luis bura amesema kwa sasa wameanza utaratibu mpya wa kuwapokea wakimbizi kutoka Burundi ambapo sasa wanahojiwa kabla ya kupewa hadhi ya ukimbizi.

Source: ITV
Burundi yawataka raia wake waliokimbilia nchi jirani kurejea.  Burundi yawataka raia wake waliokimbilia nchi jirani kurejea. Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 01:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.