Loading...

Ushauri wa bure alioutoa Frank Lampard kwa Chelsea

FRANK LAMPARD ameionya Klabu yake ya zamani ya Chelsea juu ya msimu ujao wa uhamisho.

Lampard amesema kuwa itakuwa ni jambo gumu au lisilowezekana kumpata mbadala wa haraka katika nafasi ya mshambuliaji Diego Costa kama ataamua kuondoka Stanford Bridge katika majira ya joto.

Costa amekuwa akigonga vichwa vya habari akihusishwa na kuondoka Chelsea na kwenda Atelico au kwenda Ligi kuu ya China, ambapo habari zote hizo hazijathibitishwa.

Hata hivyo, kufuatia suala hilo, Mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard ametoa ushauri wake kuhusiana na hali nzima ilivyo.

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya Chelsea endapo watachukua uamzi wa kumuacha Costa, Lampard aliiambia 'Sky Sports' mapema mwezi huu kuwa: "Itakuwa ni ngumu sana....
"

"Hapo unazungumzia juu ya washambuliaji wa ngazi ya juu. Unapojaribu kufikiria kuhusu washambuliaji hao ni vigumu sana kuwapata.

"Ukiangalia katika Ligi Kuu, utampata Harry Kane na Romelu Lukaku. Unaweza usiwe na uwezo wa kuwasajili [mmoja wao] na kama basi utawasajili itakubidi kulipa fedha nyingi mno.

"Nadhani Chelsea watahitaji kuendelea naye. Hapo suala linabaki kwake yeye [
Diego Costa], kama anataka kubaki au vinginevyo. "
Ushauri wa bure alioutoa Frank Lampard kwa Chelsea Ushauri wa bure alioutoa Frank Lampard kwa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 3/29/2017 03:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.