Loading...

VIDEO: Christiano Ronaldo alivyoinusuru Real Madrid kufungwa na klabu ya Las Palmas kwenye La liga

Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kusawazisha Real Madrid dakika ya 89 katika sare ya 3-3 na Las Palmas kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Ronaldo alifunga mabao mawili jana, lingine kwa penalti dakika ya 86, wakati bao lingine la Real Madrid iliyokuwa pungufu baada ya winga wake, Gareth Bale aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47, lilifungwa na Isco dakika ya 8.

Magoli ya Las Palmas yalifungwa na Tana Dominguez dakika ya 10, Jonathan Viera kwa penalti dakika ya 56 na Kevin-Prince Boateng dakika ya 59. Kwa matokeo hayo, Real inaangukia nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga kwa pointi zake 56 za mechi 24, ikiipisha juu Barcelona yenye pointi 57 za mechi 25.

VIDEO: Christiano Ronaldo alivyoinusuru Real Madrid kufungwa na klabu ya Las Palmas kwenye La liga VIDEO: Christiano Ronaldo alivyoinusuru Real Madrid kufungwa na klabu ya Las Palmas kwenye La liga Reviewed by Zero Degree on 3/02/2017 04:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.