Loading...

VIDEO: Goli bora la mwezi February katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]

Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard ndiye aliyeshinda tuzo ya bao bora ya Februari katika Ligi Kuu England.

Bao la Hazard alilofunga katika mechi dhidi ya Arsenal ndiyo limeibuka na ubora huo.



Katika mechi hiyo, Chelsea iliitwanga Arsenal kwa mabao 3-1.


Wakati huo huo, kocha wa klabu ya soka ya Manchester City, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari katika ligi ya Uingereza.


Guardiola ameshinda tuzo hiyo baada ya timu yake kufanya vizuri katika michezo ya ligi waliocheza ndani ya mwezi huo na kupata matokeo mazuri ikiwemo 4-0 West Ham (ugenini), 2-1 dhidi ya Swansea (nyumbani) na 2-0 dhidi ya Bournemouth (ugenini).



Naye Harry Kane wa Tottenham Hospurs amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwenye ligi hiyo.
VIDEO: Goli bora la mwezi February katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] VIDEO: Goli bora la mwezi February katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] Reviewed by Zero Degree on 3/10/2017 11:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.