Tanzania yang'ara nchini Ujerumani
Banda la Tanzania katika maonyesho ya Kimataifa ya ITB yanayoendelea Berlin, Ujerumani limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonyesho hayo.
Banda hilo lina vivutio mbalimbali ikiwemo michoro na nyayo za binadamu wa kale (zamadamu) pamoja na historia yake ikikonga mioyo ya wageni hao.
Vivutio vingine muhimu vya Tanzania ni katika maonyesho hayo ni michoro ya Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Devota Mdachi amesema pamoja na utangazaji mkubwa wa vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania unaofanywa katika maonesho haya, TTB imeamua kuweka mkazo maalumu katika kuitangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu kwa kuleta vielelezo vinavyothibitisha ukweli huo ikiwa ni pamoja na nyayo ya binadamu wa kale iliyogunduliwa huko Laetoli.
“Nyayo za Laetoli kama ilivyo kwa fuvu la binadamu wa kale lililovumbuliwa huko Olduvai Gorge, ni uthibitisho wa binadamu wa kale kuishi Tanzania, hivyo tunafurahi kuwa michoro na nyayo tulizokuja nazo zimewavutia sana wageni na dhamira yetu ni kwamba dunia ijue ukweli huo” amesema Mdachi.
Jumla ya makampuni 61 kutoka taasisi za umma na binafsi kutoka Tanzania zinashiriki maonesho ya ITB mwaka huu chini ya usimamizi TTB.

Reviewed by Zero Degree
on
3/10/2017 11:51:00 PM
Rating: