Tahadhari: Jeshi la polisi limetoa tahadhari kwa wananchi juu ya utapeli unaofanyika kwa njia ya mtandao.
Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro |
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro imesema matapeli hao ambao hutumia njia ya mtandao wamekuwa wakitumia tovuti iitwayo www.vocobaloanstz.wapka_mob ambapo katika ukurasa wa facebook wa tovuti hiyo picha inayoonekana ni ya Dkt Reginald Mengi huku pia ikiwa na nambari za simu za 0757 308 381//0768 199359.
Kamishina Sirro amewataka wananchi kutokuwa wepesi wa kukubali matangazo ya mikopo yanayotolewa kupitia mitandao ya kijamii ambapo mpaka sasa Bw. Bonifas Samson amekwisha kutiwa nguvuni baada ya kubainika kuwa miongoni mwa matapeli ambao wanahusika na saccos hiyo ya kitapeli iitwayo focus vicoba.
Katika hatua nyingine taarifa hiyo ya jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha mbili aina ya shortgun na pump action zikiwa na risasi moja ikiwa ni pamoja na magari mawili yaliyokuwa yakihusishwa na vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Source: ITV
Tahadhari: Jeshi la polisi limetoa tahadhari kwa wananchi juu ya utapeli unaofanyika kwa njia ya mtandao.
Reviewed by Zero Degree
on
3/10/2017 11:58:00 PM
Rating: