Loading...

VIDEO: Jinsi Eden Hazard na Diego Costa walivyoipaisha Chelsea jana dhidi ya West Ham United

Wachezaji Diego costa na Eden Hazard wamezidi kuipaisha kileleni chelsea kwa ushindi wa mabao 2 kwa 1 katika mchezo wao dhidi ya West Ham United ligi kuu ya England.

Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kuzitikisa Kamba za West Ham katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza kwa bao la Eden Hazard, baadaye Diego Costa akawachapa Weat Ham bao la pili na la mwisho katika dakika ya 50 kwenye kipindi cha pili.

West Ham United walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kwa goli la Manuel Lanzini dakika ya (90+2)

Kwa ushindi huo Chelsea wamefikisha alama 66 na kuicha Tottenham iliyopo nafasi ya pili kwa alama 10, huku Manchester city,Liverpool , Arsenal na Manchester United zikijikongoja kwa mwendo wa kinyonga.

Ushindi huo pia kwa Chelsea ni dalili nyeupe ya kutwaa taji la ligi kuu England msimu wa 2016/17 kwa kuwa hakuna dalili za timu yoyote kuweza kufikisha idadi ya alama ambazo tayari Chelsea wamejikusanyia.

Katika timu ambazo zimeonyesha njia ya kushuka daraja kwa kuwa na alama ndogo kuliko timu zote ni Sunderland ambao ndio wanaburuza mkia katika msimamo kwa alama 19,wakifuatiwa na Hully city yenye alama 21 na Midllesbrough yenye alama 22.


VIDEO: Jinsi Eden Hazard na Diego Costa walivyoipaisha Chelsea jana dhidi ya West Ham United VIDEO: Jinsi Eden Hazard na Diego Costa walivyoipaisha Chelsea jana dhidi ya West Ham United Reviewed by Zero Degree on 3/07/2017 11:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.