Loading...

VIDEO: Mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018, ...Brazil ilivyoilaza Uruaguay kwa ushindi wa goli 4-1

Timu ya taifa ya Brazil wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Uruguay kwa mabao 4-1. katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018.

kiungo Paulinho akifunga hatrick na Neymer akifunga bao moja, huku bao pekee la Uruguay likifungwa na mshambuliaji Edson Cavan kwa mkwaju wa penati.



Katika michezo Colombia waliibuka na ushinda kwa bao 1 - 0 dhidi ya Bolivia goli la Colombi, likiwekwa kambani na mshambuliaji mahiri wa timu hiyo James Rodrigues.

Argentina wakapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile. Bao pekee la Argentina likifungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati.

Paraguay wakawachapa Ecuador 2-1. Nao Venezuela wakatoshana nguvu na Peru kwa sare ya 2 - 2.



Michezo ya kufuzu kombe la dunia leo:

Leo katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018 kwa kanda ya ulaya nyasi za viwanja tisa zitawaka moto  .

Michezo ya kundi D Georgia watacheza na Serbia, Austria watakua wenyeji wa Moldova na Ireland wakicheza na Wales.

Katika kundi G Hispania watakipiga na Israel, Liechtenstein wao watapimana ubavu na Macedonia, waitaliano wao watakipiga na Albania.

Croatia wao watakua wenyeji wa Ukraine, huku Kosovo wakicheza na Iceland nao Finland wakiwa ugenini dhidi ya Uturuki hii ikiwa ni michezo ya kundi I
VIDEO: Mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018, ...Brazil ilivyoilaza Uruaguay kwa ushindi wa goli 4-1 VIDEO: Mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018, ...Brazil ilivyoilaza Uruaguay kwa ushindi wa goli 4-1 Reviewed by Zero Degree on 3/24/2017 10:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.