Waziri alaani kitendo cha askari kuchomoa bastola wakati wakimdhibiti Nape Nnauye
- Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ....Nape 'Out', Mwakiembe kujaza nafasi yake
- Mkutano wa Nape wazuiwa Protea, ...azungumza na wanahabari chini ya ulinzi wa polisi
- Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa athibitisha Rais kumteua Dk. Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye
Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.
Nchemba, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
"Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini," ameandika.
"Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
- Ningeteuliwa kuwa Waziri ningeanzisha mpango maalum wa kuwachuja wasanii, RAY
- Mimi ndio chanzo kikubwa cha Nape kuvuliwa uwaziri, Gwajima
"Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini," ameandika.
"Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
Source: BBC Swahili
Waziri alaani kitendo cha askari kuchomoa bastola wakati wakimdhibiti Nape Nnauye
Reviewed by Zero Degree
on
3/24/2017 09:54:00 AM
Rating: