Loading...

Ningeteuliwa kuwa Waziri ningeanzisha mpango maalum wa kuwachuja wasanii, RAY

MKONGWE wa filamu Nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’, amefunguka kuwa kama angeteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, angeanzisha mpango maalumu wa kuwachuja wasanii.

Akiongea na +225 Kipindi cha XXL cha Clouds Fm amedai kuwa kila mtu anataka kuwa msanii, hakuna mgawanyiko wa kazi. Msanii akicheza filamu moja basi kesho ameshakuwa staa na anavaa kofia zote kama vile utayarishaji, uongozaji na uigizaji.

Ray amekerwa sana na jambo hilo pia amemshauri Dk. Harrison Mwakyembe kuwa aliangazie soko la filamu Bongo kwani sinema za kizungu zinauzwa shilingi 700 na filamu za hapa Bongo ni shilingi 2500.

Ray amedai kuwa filamu hizo zinauzwa gharama hiyo kwa kuwa zinauzwa bila ya kulipiwa kodi.
Ningeteuliwa kuwa Waziri ningeanzisha mpango maalum wa kuwachuja wasanii, RAY Ningeteuliwa kuwa Waziri ningeanzisha mpango maalum wa kuwachuja wasanii, RAY Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.