Loading...

VIDEO: Stars walivyotoka kifua mbele Taifa kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Botswana

Timu ya Tanzania, ‘Taifa Stars imeifunga Botswana mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Mabao ya Mbwana Samatta yalitosha kuwafuta machozi mashabiki wa soka nchini baada ya kufunga dakika ya 2 na 87 katika mchezo huo.



Botswana walifanya mashambulizi kadhaa katika dakika ya 22 na 27 na kufanikiwa kupata kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.




Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye alizua shangwe uwanjani hapo alipoingia na kuwapungia mkono mashabiki.



VIDEO: Stars walivyotoka kifua mbele Taifa kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Botswana VIDEO: Stars walivyotoka kifua mbele Taifa kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Botswana Reviewed by Zero Degree on 3/26/2017 12:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.