Loading...

Wafanyabiashara wasusa kuuza vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi nchini India

Maelfu ya maduka katika jimbo la Tamid Nadu nchini India yatasitisha uuzaji wa vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi kuanzia Jumatano.

Mashirika mawili ya biashara yametoa wito kwa washirika wake kususia kuuza vinywaji vya kigeni na badala yake kukuza bidhaa zinazotengezwa nchini humo.

Wameshutumu kampuni za vinywaji hivyo kwa kutumia vibaya maji nchini humo wakati ambapo wakulima wanakabiliwa na hali ngumu ya ukame.

Hatua hiyo pia inaangazia ushawishi wowote wa kigeni nchini humo.

Shirika moja linaloshirikisha kampuni za Coke na Pepsi, na shirika la vinywaji nchini humo limesema kuwa limesikitishwa sana na hatua hiyo.
Wafanyabiashara wasusa kuuza vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi nchini India Wafanyabiashara wasusa kuuza vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi nchini India Reviewed by Zero Degree on 3/01/2017 12:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.