Loading...

Wanasayansi wagundua kiumbe kingine chenye uwezo wa kubadili rangi kama Kinyonga

Unaweza kutoamini lakini inapofikia wakati ikathibitishwa ni lazima kuamini. Tumekuwa tukiamini kwa kusikia na wakati mwingine kwa kuona kwa macho yetu kuwa Kinyonga ndiye kiumbe Pekee anayeweza kubadilisha rangi yake kulingana na mazingira.

Kutana na hawa wanasayansi wa Argentina ambao wamemgundua Chura wa kwanza duniani mwenye uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi yake anapopigwa na mwanga wa jua ambapo wanasayansi hao walisema Chura huyo hubadilika kutoka rangi ya Kahawia kwenda rangi ya Kijani iliyofifia au Blue pindi anapokutana na mwanga mkali wa jua.


Wanasayansi hao walisema Chura huyo hukoza rangi zaidi anapokutana na jua kali zaidi na rangi yake huzidi kupungua akipigwa na mwanga mdogo wa jua wakidai ni jambo ambalo hawakulitegemea ukiwa ni ugunduzi mpya kwao kwa kuwa ni mara chache viumbe wa ardhini kuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi zao.
Wanasayansi wagundua kiumbe kingine chenye uwezo wa kubadili rangi kama Kinyonga Wanasayansi wagundua kiumbe kingine chenye uwezo wa kubadili rangi kama Kinyonga Reviewed by Zero Degree on 3/16/2017 01:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.