Loading...

Wauza asali wapewa mwezi 1 kuacha kutumia machupa ya konyagi kuuzia bidhaa hiyo

Wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikungi, mkoani Singida waliopo kando kando ya barabara kuu Singida-Dodoma, wamepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa, kutumia vifungashio halisi badala ya chupa za konyagi, ili kulinda afya za walaji.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturi, ametoa agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa matumizi sahihi ya vifungashio vya asali, iliyofanyika katika kijiji cha Issuna tarafa ya Ikungi.

Alisema ufungaishaji wa asali unaofanywa na wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikaungi, sio wa kuridhisha na kwa namna moja au nyingine, unachangia kuharibika kwa asali.

“Ufungaishaji unao fanywa na wafugaji wetu wa nyuki,unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa soko la asali.Wafanyabiashara hawa wanaouzia asali pembezoni mwa barabara,wanafungasha asali bila kuzingatia sheria na kanuni za biashara ya mazao ya nyuki hususani asali.Nawapeni mwezi moja mbadilike katika ufungaishaji,” alisisitiza Mtaturu.

Mkuu wa wilaya hiyo, pia amewataka wauzie asali ndani ya jengo maalumu la kuuzia mazao ya nyuki ambalo toka limalizike kujengwa mwaka 2013, hadi sasa halijawahi kutumiwa.

Awali kaimu meneja wakala wa huduma za misitu wilaya ya Ikungi, Samson Lyimo,alisema asilimia 70 ya eneo la ardhi ya wilaya ya Ikungi ni misitu, miti, vichaka na nyanda za mbunga, ambayo ni rasilimali muhimu kwa ufugaji wa nyuki.

Hata hivyo, Lyimo, alisema ni asilimia ndogo ya eneo hilo linalotikika kwa shughuli za ufugaji nyuki.

“Ufugaji wa nyuki wilaya ya Ikungi,unafanywa na mtu mmoja mmoja na wengine wamejiunga katika vikundi na kufanya shughuli kwa pamoja. Hadi sasa tunayo vikundi 63 ambavyo vimesajili na vinajihusisha na uzalishaji wa mazao ya nyuki ambayo ni asali na nta,” alisema kaimu meneja huyo.

Lyimo alisema kuwa asali ambayo imezalishwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za ufugaji, ikachakatwa vizuri, ikafungaswa vizuri na kuwekewa lebo, ina soko zuri ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, alisema kuwa ubora wa asali ya wilaya ya Ikungi, unaathiriwa na mambo mengi ikiwemo ya wafungaji kuvuna asali ambayo haijakomaa.

“Wafungaji wengine wanachemsha asali baada ya kuivuna, wengine kuchanganya na maji,kuongezea asali na kuuzia barabarani kwenye joto kali,” alisema.

Akisisitiza, alisema baadhi ya wafanyabiashara huweka asali kwa kutumia vyombo ambavyo tayari vimeishatumika kufungashia bidhaa zingine kama pombe viuatilifu, maji na mafuta ya aina mbalimbali.

Lyimo alisema matumizi ya vifungaishia hivyo,ni kinyjme na kanuni za ufugaji nyuki ya 2005 sehemu ya III, kifungu cha 21 (4) (a-i).

Baadhi ya wajasiriamali, akiwemo Musa Mwanja na Nasson Lucas wameomba muda zaidi wa kujiandaa.

Hata hivyo,lmkurugenzi mtendaji halmashauri wilaya ya Ikungi, Rustika Turuka, anasema agizo hilo litatekelezwa ili kulinda soko na afya za walaji.

Uzalishaji wa mazao ya asali, hususani asali umekuwa ukiongezeka Wilayani Ikungi kutoka tani 3.74 mwaka 2015/16 hadi kufikia tani 4.416 mwaka 2016/17.
Wauza asali wapewa mwezi 1 kuacha kutumia machupa ya konyagi kuuzia bidhaa hiyo Wauza asali wapewa mwezi 1 kuacha kutumia machupa ya konyagi kuuzia bidhaa hiyo Reviewed by Zero Degree on 3/05/2017 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.