Loading...

Yaliyosemwa na msemaji wa Bunge baada ya kujiuzulu kwa viongozi wa Kamati ya Viwanda na Biashara

Msemaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Owen Mwandumbya
Mwandumbya amesema kuwa ofisi ya Bunge imepokea barua ya kujiuzulu kwa viongozi wa Kamati ya Viwanda na Biashara kwa nafasi ya Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara, Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, mapema leo kufuatia barua yao hiyo ya kujiuzulu.

Bwana amebainisha kuwa, tayari ofisi ya Bunge imepokea barua yao hiyo na kueleza kuwa, Wajumbe wa Kamati hiyo wanayo nafasi ya kuchagua viongozi wapya.

“Barua ya viongozi wa Kamati kujiuzulu tumeipata. Kwa suala la kuziba nafasi lipo kwa wajumbe wenyewe wa Kamati ambao wataweza kuchaguana na kisha kutoa taarifa kwa Spika” alifafanua msemaji wa Bunge.

Mapema leo Machi 20.2017, Viongozi hao wa Kamati ya viwanda na biashara waliandika barua yao ya kijiuzulu nafasi zao kwa maelezo kuwa Serikali inaingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo hawaoni sababu za kuendelea huku wakikabidhi barua yao hiyo ya kujihuzuru ofisi ya spika.

Barua ya kujiuzulu nafasi hizo

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara, Dk Dalali Kafumu aliyejiuzulu kamati hiyo

Aliyekuwa Makamu wa kamati hiyo ya Viwanda na Biashara, Mh. Vick Kamata
Source: DewjiBlog
Yaliyosemwa na msemaji wa Bunge baada ya kujiuzulu kwa viongozi wa Kamati ya Viwanda na Biashara Yaliyosemwa na msemaji wa Bunge baada ya kujiuzulu kwa viongozi wa Kamati ya Viwanda na Biashara Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 11:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.