Loading...

FIFA yamfungia kuchezesha soka mwamuzi toka nchini ya Ghana

Mwamuzi raia wa Ghana Joseph Lamptey, amepigwa marufuku ya maisha na shirikisho la kandanda Duniani (Fifa), baada ya masuali kuibuka jinsi alivyochezesha mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Senegal na Afrika Kusini Novemba iliyopita.

Afrika Kusini ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1 lakini Senegal ikalalamika kwa shirikisho la Fifa.

Walisema kuwa Lamptey aliwapa Afrika kusini penalti licha ya naibu refa kuashiria kuwa ingekuwa kona.

Wengi waliuliza maswali kuhusu kona hiyo wakati huo, kikiwmeo kitengo cha michezo cha BBC kilichoripoti kuwa Afrika Kusini iliongoza baada ya panelti hiyo yenye utata.
FIFA yamfungia kuchezesha soka mwamuzi toka nchini ya Ghana FIFA yamfungia kuchezesha soka mwamuzi toka nchini ya Ghana Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 11:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.