Loading...

Waziri Nape amelaani kitendo cha Mkuu wa mkoa wa Dar kuvamia ofisi za Clouds Media.

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mh Nape Nnauye amelani tukio la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda la kuvamia ofisi za Clouds Media jijini Dar es Salaam siku ya ijumaa usiku na kwamba tukio hilo limeweka doa uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za Clouds Media Mikocheni jijini Dar es Salaam, waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi kutoka TCRA, mkurugenzi wa habari maelezo na mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania Dr. Reginald Mengi ambapo mbali na kuwapa pole uongozi na wafanyakazi wa Clouds Media kwa kile kilichotokea,Nape amesema kama serikali wanakilani tukio hilo kwa nguvu zote.

Kutokana na tukio hilo,waziri Nape Nnauye akalazimika kuunda kamati ya watu watano watakaofanya kazi hiyo kwa saa 24 ili kutoa nafasi ya kamati hiyo kupata maelezo ya upande wa pili ili wa mkuu wa mkoa wa DSM naye apewe nafasi ya kujieleza.

Aidha mwenyekiti wa MOAT ameomba hatua zichukuliwe baada ya kamati hiyo kumaliza kusikiliza upande wa pili.
Waziri Nape amelaani kitendo cha Mkuu wa mkoa wa Dar kuvamia ofisi za Clouds Media. Waziri Nape amelaani kitendo cha Mkuu wa mkoa wa Dar kuvamia ofisi za Clouds Media. Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 11:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.