Loading...

Aliyekuwa kiongozi wa 'Freemason' azikwa kwa kuchomwa moto

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Freemason Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Andy Chande, umeteketezwa leo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kupitia tukio lililodumu kwa takribani saa moja.

Mwili huo umeteketezwa kwa moto kupitia ibaada iliyofanyika kwenye nyumba maalumu inayotumika kama sehemu ya maziko ya waumini wa dini ya Hindu.

Sir Chande alifariki dunia siku tano zilizopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa ulitokana na matatizo ya utumbo mdogo kusambaza sumu mwilini.



Aliyekuwa kiongozi wa 'Freemason' azikwa kwa kuchomwa moto Aliyekuwa kiongozi wa 'Freemason' azikwa kwa kuchomwa moto Reviewed by Zero Degree on 4/11/2017 06:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.