Loading...

Ben Pol na Songa waibuka washindi wa tuzo za Mdundo

Kwa mara ya kwanza, kampuni ya muziki ya Mdundo.com inayowezesha mashabiki kupakua nyimbo mbalimbali za wasanii wa muziki hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla, Ijumaa hii, Machi 31, 2017 imefanikiwa kutoa tuzo kwa wasanii ambao wameshinda kutokana na wingi wa upakuaji wa nyimbo zao.

Katika tuzo hizo wasanii waliopata ushindi ni pamoja na Ben Pol ambaye amefanikiwa kuchukua tuzo mbili, Msanii wa bora wa Afropop pamoja na wimbo bora uliopakuliwa zaidi, huku tuzo ya msanii bora wa hiphop ikichukuliwa na Songa. Washindi hao walipata nafasi ya kujumuika pamoja na kupata chakula cha mchana katika maeneo ya Masaki kwenye kiota cha Alcove Restaurant.

Tuzo hizo ambazo zilikuwa zinawaniwa na wasanii mbalimbali, zilikuwa kwenye vipengele vikuu vitatu:

Kipengele cha wimbo ulio pakuliwa zaidi:

Washiriki:

1: Enzi Za UtotoSonga
2: ForeverRuby
3: JuuJux and Vanessa
4: KamatiaNavy Kenzo
5: Mahaba NiueMaua Sama
6: Moyo MashineBen Pol
7: SiweziBraka Da Prince
8: SkendoMo Music
9: Uzuri WakoJux

Songa akiwa na Meneja wake, Chin

Tuzo 3 ambazo Ben Pol na Songa wameshinda
Kipengele cha Msanii bora wa Hip Hop:

1: Chindo Man
2: Dizasta
3: Gnako
4: Godzilla
5: Nikki Mbishi
6: One The Incredible
7: P The Mc8: Songa
9: Young Killer

Kipengele cha Msanii Bora wa Afropop:
Washiriki:

1: Barakah Da Prince
2: Belle 9
3: Ben Pol
4: Christian Bella
5: Jux
6: Maua Sama
7: Mo Music
8: Navy Kenzo
9: Ruby
10: Vanessa


Ben Pol na Songa waibuka washindi wa tuzo za Mdundo Ben Pol na Songa waibuka washindi wa tuzo za Mdundo Reviewed by Zero Degree on 4/01/2017 03:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.