Loading...

Msigwa: Tuko imara hatuyumbishwi na wanaohamia CCM

Mhe. Peter Msigwa
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amewaaminisha wafuasi wa chama hicho mkoani humo kuwa kipo imara na wala hakiteteleki na ongezeko la wimbi la madiwani na wabunge wao wanaohamia Chama cha Mapinduzi.

Msigwa amesema iko haja ya wananchi kuwapuuza viongozi hao wanaohama vyama kwani wameshindwa kuwa na utu na kuheshimu heshima kubwa waliyopewa na Watanzania kuwaongoza na badala yake wanakimbia majukumu.

“Hao watu ni wa kupuuzwa na wala hii si habari mpya kwetu tunajua nini wanafanya lakini niwaambie wana Iringa mimi na chama changu tuko imara hatuyumbishwi na hao wachache wanaoondoka na tutaendelea kuwatumikia kwa moyo mmoja,” amesema Mchungaji Msigwa kwenye mahojiano yake na gazeti la Mtanzania.

Mhe. Msigwa amesema hayo ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya Diwani wa Kata ya Gangilonga ambaye pia alikuwa ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Dady Igogo kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo ya udiwani na kuwa raia wa kawaida.

Katika hali ya kushangaza Igogo ameeleza kuwa sababu za kujiuzulu kwake ni kutokana na kupitia kipindi kigumu kwenye siasa pia ni faida kwa usalama wa maisha yake.
Msigwa: Tuko imara hatuyumbishwi na wanaohamia CCM Msigwa: Tuko imara hatuyumbishwi na wanaohamia CCM Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 08:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.