Loading...

Zitto Kabwe aitwa Polisi Mororgoro


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameitwa katika Kituo cha Polisi cha Mgeta wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro kwa ajili ya mahojiano.

Mbunge huyo wa Jimbo la Kigoma Mjini yupo katika ziara ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Taarifa ya MCL Digital, Zitto amesema ametakiwa kuripoti katika kituo hicho baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), kuagiza aende.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari yenye kichwa cha habari ‘Tuko Kikeo, polisi wametuvamia’, Zitto amesema, “Tumemaliza ziara yetu ya kutembelea Kata ya Kikeo, inayoongozwa na diwani wa chama cha ACT Wazalendo, hapa Halmashauri ya Mvomero, mkoa wa Morogoro.” 

“Polisi wametuvamia jioni hii, hawajatueleza wanachokitaka. Tunakwenda nao Kituo cha Polisi Mgeta muda huu kuwasikiliza.”
Zitto Kabwe aitwa Polisi Mororgoro Zitto Kabwe aitwa Polisi Mororgoro Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 08:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.