Loading...

Mwili wa Akwilina waagwa jijini Dar es Salaam


Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi juma lililopita, Akwelina Akwilini umeagwa na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi siku ya Ijumaa wiki hii.

Katika ibada ya heshima za mwisho ilyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT hapo Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo Akwelina Akwilini, na kumuweka wazi ili awaombe radhi Watanzania.

Picha ya Akwelina Akwilini ilipambwa na maua katika ibada ya kuaga mwili wake
Akwilina Akwilini alipigwa risasi na Polisi juma lilopita siku ya Ijumaaa wakati kikosi cha polisi kitengo cha kutiliza ghasia,FFU, kilipokuwa kikiwakabili waaandamanaji wa chama cha upinzani cha CHADEMA baada ya kumaliza Kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni,jijini Dar es salaam.


Katika ibada hiyo pia liliibuka kundi la wanafunzi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakitaka haki itendeke, mabango ambayo waliyainua punde Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako alipo anza kuzungumza. Lakini pingamizi lao likasitishwa na askari waliochukua mabango hayo na kuyachana.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa asasi za kiraia, wanaharakati wa haki za binadamu na chama cha taifa cha wanafunzi za kumtaka Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba.

Hadi sasa polisi 6 wanaodaiwa kuhusika katika kuuwawa kwa manafunzi huyo wametiwa mbaroni.

Mamia ya Watanzania wajitokeza kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT kuaga mwili wa mwanafunzi
Maadhimisho Haya ya ibada misa takatifu yamehudgiriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali wakimwo Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Hamad Masauni.
Mwili wa Akwilina waagwa jijini Dar es Salaam Mwili wa Akwilina waagwa jijini Dar es Salaam Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 06:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.