Loading...

Dybala haijui 'future' yake Juve, ...hili ndilo jibu lake juu ya tetesi za kutaka kuhamia Chelsea

Nyota anayewika kwa sasa akiwa na klabu ya Juventus, Paulo Dybala anasema 'hajui nini hatima yake katika klabu hiyo kwa baadaye' huku kukiwa na uvumi mkubwa unaomhusisha na kuhamia Chelsea msimu ujao.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argetnina amefanikiwa lufunga mabao 37 katika michezo 78 akiwa Juve tangu alipojiunga na vigogo hao wa Italia mwaka 2015, lakini amekuwa akihusishwa na kuhamia 'The Blues' tangu Antonio Conte aliposajiwa kuwa meneja wa timu hiyo ya London.

Inajulikana kuwa Dybala mwenye umri wa miaka 23 ni kipenzi cha Conte na bado hakuna uhakika wa kwamba atasaini mkataba mpya na Juve.

Kuhusiana na uvumi unaomhusisha na kuhamia Stamford Bridge, Dybala aliliambia 'La Repubblica': 

"Siijui 'future', hivyo ni mambo mengi yanayoweza kutokea.

"Ninafuraha, wachezaji wenzangu wananitakia mema, hata na mashabiki wa klabu pia wananitakia mema.

"Kwa wakati huu najisikia vizuri nikiwa hapa."

Barcelona pia imeonyesha nia ya kumtaka Dybala msimu huu, huku akitabiliwa kuja kufikia uwezo kama wa Lionel Messi katika siku zijazo.
Dybala haijui 'future' yake Juve, ...hili ndilo jibu lake juu ya tetesi za kutaka kuhamia Chelsea Dybala haijui 'future' yake Juve, ...hili ndilo jibu lake juu ya tetesi za kutaka kuhamia Chelsea Reviewed by Zero Degree on 4/13/2017 12:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.