FIFA, CAF wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwenye michezo ya kimataifa
Siku kadhaa zimepita toka club ya Dar es Salaam Young Africans ikataliwe na shirikisho la soka Tanzania TFF kuutumia uwanja wa CCM Kirumba katika mechi dhidi ya MC Alger iliyochezwa April 8 uwanja wa Taifa kwa kigezo kuwa uwanja huo hauna vigezo.
Hatua hiyo imetangazwa Ijumaa hii na Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi. “Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa,” ametweet Malinzi.
Kupitishwa kwa uwanja huo kumekuja baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kwenda Mwanza kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana.
Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.
Viwanja vingine ambavyo vimekaguliwa na vinasubiri kupitishwa ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.
Kwa kawaida mechi za kimataifa zinaruhusiwa kuchezwa katika viwanja vyenye viwango na vilivyoidhinishwa na FIFA na CAF lakini CCM Kirumba haikuwa imepitishwa hivyo Yanga kushindwa game vs MC Alger CCM Kirumba.
Good news ikufikie aliyoitangaza leo Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter ni kuwa CAF na FIFA wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba utumike katika mechi za kimataifa, hivyo timu za Tanzani zitakuwa na uhuru wa kutumia uwanja wa Taifa au Kirumba.
Good news ikufikie aliyoitangaza leo Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter ni kuwa CAF na FIFA wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba utumike katika mechi za kimataifa, hivyo timu za Tanzani zitakuwa na uhuru wa kutumia uwanja wa Taifa au Kirumba.
Hatua hiyo imetangazwa Ijumaa hii na Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi. “Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa,” ametweet Malinzi.
Kupitishwa kwa uwanja huo kumekuja baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kwenda Mwanza kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana.
Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.
Viwanja vingine ambavyo vimekaguliwa na vinasubiri kupitishwa ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.
FIFA, CAF wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwenye michezo ya kimataifa
Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2017 10:22:00 AM
Rating: