Loading...

Fundi apandishwa kizimbani kwa kosa la 'kuflashi' simu zilizofungiwa na TCRA

FUNDI simu za mkononi, Juma Maulid (30) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya kuzifungua simu tano zilizofungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alidai kuwa Novemba 8, mwaka jana eneo la Kariakoo, Mtaa wa Agrey, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alighushi na kuzifungua simu tano.

Mkunde alizitaja simu hizo kuwa ni aina ya Tecno zilizokuwa zimefungiwa na TCRA kutokana na kutokuwa na ubora kwa matumizi ya binadamu.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Hakimu alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni tano kila mmoja.

Mshtakiwa alitimiza masharti hayo na kesi hiyo itatajwa Mei 5.
Fundi apandishwa kizimbani kwa kosa la 'kuflashi' simu zilizofungiwa na TCRA Fundi apandishwa kizimbani kwa kosa la 'kuflashi' simu zilizofungiwa na TCRA Reviewed by Zero Degree on 4/22/2017 10:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.