Loading...

Barua ya Simba ya kuomba maandamano ya amani wakidai hawatendewi haki na TFF

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva
Taarifa ni kuwa Klabu ya Simba imeomba kuandamana kuelekea kwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Aveva, Harrison Mwakyembe kutokana na kudai kuwa hawatendewi haki na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).

Barua ambayo inaonekana imesainiwa na Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva kuelekea kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro kuomba kufanya maandamano ya amani kupinga walichodai ni uonevu wa TFF.

Nakala ya barua hiyo nakala yake imetumwa kwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo ambapo wameoba maadamano hayo yafanyike Jumanne ya Aprili 25, 2017.

Katika barua hiyo Aveva ameeleza kuwa wanaomba maandamano hayo yatakayohusisha wanachama wote wa Simba, yaanzie makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi hadi Wizara ya Habari.

Aidha, Aveva amesema wana taarifa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameitwa kwenye Kamati ya Maadili kwa kile kinachoonekana kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asiweze kuongeela uonevu huu.

Maombi hayo yanakuja muda mfupi baada ya TFF kumtaka Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara kufika Kamati ya Maadili Aprili 21, 2017 kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu dhidi ya viongozi wa shirikisho hilo.

Hivi karibuni kumekuwa na mzozo wa pointi za mezani ambazo Simba ilipewa kutoka katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kudaiwa kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alitumika akiwa na kadi tatu za njano.


Barua ya Simba kuomba maandamano ya amani
Barua ya Simba ya kuomba maandamano ya amani wakidai hawatendewi haki na TFF Barua ya Simba ya kuomba maandamano ya amani wakidai hawatendewi haki na TFF Reviewed by Zero Degree on 4/22/2017 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.