Hashim Rungwe akosoa uteuzi wa Rais John Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amekosoa uteuzi wa Rais John Magufuli wa kuteua watendaji wengi kutoka chama chake cha CCM na kuwaacha wengine.
Rungwe ameyasema hayo katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kitungo cha runinga cha ITV alipoalikwa kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yanahusu maisha yake ya siasa.
Alisema kuwa ni vyema Rais akawa anafanya uteuzi kutoka vyama vyote kwani hata wanavyama wa vyama vingine vya siasa wana uwezo na wamesomeshwa kwa pesa za serikali.
Aidha Rungwe alipongeza uteuzi wa Rais Magufuli kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji lakini akiongeza kuwa Rais alichelewa kufanya uteuzi huo.
“Hawa watu wote wamesoma kwa pesa ya serikali kwa hiyo ni sahihi kwake kuteua kutoka pande zote … uteuzi wa Prof. Mkumbo kutoka ACT ni mzuri lakini alichelewa maana sasa anaenda mwaka wa pili ndiyo anachukua mtu wa upinzani,” alisema Rungwe.

Reviewed by Zero Degree
on
4/25/2017 04:01:00 PM
Rating: