Loading...

Henry ataja kocha bora wa msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal, amemtaja bosi wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte kuwa ndiye kocha bora wa msimu huu.

Antonio Conte amekuwa akisifiwa na wengi kwa kuirudisha Chelsea katika hali nzuri pale Stamford Bridge ukiachana na msimu ulioisha.

Kufuatia ushindi wao wa goli 3-1 dhidi ya Bournemouth juzi, 'The Blues' sasa wanakaa kileleni kwa pointi saba zaidi mbele ya Spurs walioko nafasi ya pili.
Mkongwe huyo wa zamani wa Arsenal, Henry amemtaja Muitaliano huyo kuwa kocha bora katika Ligi Kuu msimu huu.

"Kama kocha, Conte amefanya ambacho kocha unastahili kufanya," Henry aliiambia Sky Sports.

"Aliwasili Chelsea, akafanya tathmini ya hali na wala hakukurupuka kufanya anavyotaka tangu mwanzo.

"Yeye alifanya ambacho kocha mzuri hupaswa kufanya, na endapo kisipozaa matundu mazuri hufanya mabadiliko.

"Na imeonekana kufanya kazi kwa sababu mfumo wake umesaidia kila mchezaji kwa nafasi yake kufanya vizuri."
Henry ataja kocha bora wa msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] Henry ataja kocha bora wa msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 01:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.