Loading...

Huu ndio utabiri wa Michael Owen wa mechi ya Manchester United dhidi ya Chelsea Jumapili

Owen anatabiri mpambano kati ya Manchester United na Chelsea utamalizika kwa sare tasa katika uwanja wa Old Traford siku ya Jumapili jioni.

Kwa kuandika utabiri wake katika safu ya 'Bet Victor' kuhusu mchezo ambao utaikuta Manchester nyumbani dhidi ya Chelsea, mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Owen amedai kwamba wapinzani hao wataishia kuondoka napointi moja kila mmoja.

"Chelsea tayari wameshaifunga Manchester United mara mbili katika uwanja wa Stamford Bridge msimu huu na Jose Mourinho sidhani kama atataka klabu yake ya zamani kujiwekea uhakika wa kubeba taji la ligi pale Old Trafford siku ya Jumapili," Owen alisema.

Aliongeza: "Sitarajii kuona mchezo wa kiufundi na pengine pande zote mbili zitachukua hatua sasa."
Huu ndio utabiri wa Michael Owen wa mechi ya Manchester United dhidi ya Chelsea Jumapili Huu ndio utabiri wa Michael Owen wa mechi ya Manchester United dhidi ya Chelsea Jumapili Reviewed by Zero Degree on 4/14/2017 03:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.