Loading...

Jeshi la Marekani lapeleka meli za kivita katika rasi ya Korea

Meli ya Carl Vinson (katikati) ikisindikizwa na meli zingine
Jeshi la Marekani limetoa amri kwa meli zake za kivita zinazobeba silaha zielekee karibu na rasi ya Korea, huku kukiwa na hofu kubwa kuhusiana na Korea Kaskazini kuimarisha silaha zake za kinukilia.

Msimamizi wa kijeshi wa Marekani wa eneo la Pacific alieleza kuwa kujiandaa huko kijeshi ni muhimu katika eneo hilo.

Meli hizo zinazojulikana kwa pamoja kama The Carl Vinson Strike Group zinashirikisha meli moja kubwa ya kubeba ndege za kivita na meli zingine za kivita za kawaida.

Awali ndege hizo zilitarajiwa kuzuru Australia lakini mkondo wake ukabadiliwa kuelekea Bahari ya Pacific.

Eneo hilo la Pacific ni kule ambako wanajeshi wa Marekani walifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.

Msemaji wa jeshi la Marekani anasema kuwa Korea Kaskazini ndilo tisho kubwa zaidi kwa usalama wa eneo la Pacific.

Meli ya Carl Vinson (katikati) ikisindikizwa na meli zingine
Meli ya Carl Vinson hubeba ndege aina ya F/A-18F Super Hornets
Anasema ushahidi ni jinsi taifa hilo linavyofanya mazoezi ya zana za kinukilia kiholela.

Mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia, meli hizo za kivita zina makombora yanayoweza kuzima zana zo zote zinazolengwa kwake.
Jeshi la Marekani lapeleka meli za kivita katika rasi ya Korea Jeshi la Marekani lapeleka meli za kivita katika rasi ya Korea Reviewed by Zero Degree on 4/09/2017 06:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.