Lukaku akaribia kuvunja rekodi iliyowekwa na Henry, Tores, Ronaldo, na Suarez
Kati ya washambuliaji hatari sana msimu huu EPL ni Romelu Lukaku, msimu huu Lukaku amejenga urafiki na nyavu za wapinzani kwani hadi sasa ameshafunga magoli 23.
Magoli mawili aliyoyafunga dhidi ya Leicester City yamemfanya avunje rekodi ya nyota wa zamani wa klabu hiyo Fred Pickering aliyoiweka msimu wa mwaka 1964/1965 ya kufunga magoli 8 mfululizo katika uwanja wa nyumbani.
Lakini sii hiyo tu sasa Lukaku anakaribia kuweka rekodi mpya ambayo Thiery Henry, Luis Suarez na Cristiano Ronaldo wamewahi kuziweka katika ligi kuu ya Uingereza.
Washambuliaji hao kila mmoja ameshawahi kumaliza msimu akiwa amefunga magoli mengi kuliko moja ya timu inayoshiriki Epl, Thiery Henry msimu wa 2005/2006 alimaliza akiwa na magoli 27 ikiwa ni goli 1 zaidi ya timu ya Sunderland iliyokuwa na jumla ya magoli 26.
Mwaka 2007/2008 nao Cristiano Ronaldo alimaliza akiwa na magoli 31 huku timu nzima ya Derby Country ikimaliza msimu huo na magoli 20 yakiwa pungufu ya magoli 11 na Cristiano Ronaldo.
Luis Suarez naye 2013/2014 alimaliza msimu na magoli 31 huku timu ya Norwich ikimaliza na magoli 28, Fernando Torres naye 2007/2008 aliumaliza msimu na magoli 24 huku Derby Country wakimaliza na magoli 20.
Sasa Lukaku naye hadi sasa ana jumla ya magoli 23 lakini klabu nzima ya Middlesbrough hadi sasa wana magoli 22, endapo ligi itaisha hivi hivi na Lukaku kuzidi kufunga baasi Lukaku naye ataingia kwenye kundi moja sawa na Henry, Ronaldo, Suarez na Torres.

Reviewed by Zero Degree
on
4/11/2017 03:32:00 PM
Rating: