Loading...

Mashabiki waiweka Simba matatani kwa mara nyingine tena

Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba, kupitia Meneja wa Uwanja Ndg Steven E. Shija unapenda kutoa taarifa za uharibifu wa Uwanja.

Mechi iliyochezwa Tarehe 10.04.2017, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya Mbao Fc Vs Simba Sc umesababisha uharibifu Mkubwa kwenye Maeneo ya kuingilia Wachezaji, Waamuzi na Geti Namba 4 ambapo walikuwa wamekaa Mashabiki wa Simba.

Uharibifu huo umetokana na Mashabiki wa Timu ya Simba Sc kupanda Juu ya maeneo ya Kivuli yaliyojengwa kwenye maeneo yaliyotajwa ( Vyumba vya Kubadirishia Nguo kwa wachezaji, Waamuzi na Geti namba Nne), uharibifu huo umepelekea kushindwa kufunga Milango ya Mbele ambapo ni hatari kwa usalama wa maeneo hayo muhimu.

Hivyo uongozi wa Uwanja umeshazitaarifu Mamlaka husika ili zichukue hatua kwa Wanaohusika ili kuhakikisha eneo hilo linatengenezwa mapema kabla ya Mechi ya Toto African dhidi ya Simba Sc Tarehe 15.04.2017.




Imetolewa na:-
Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba - Mwanza
11.04.2017
Mashabiki waiweka Simba matatani kwa mara nyingine tena Mashabiki waiweka Simba matatani kwa mara nyingine tena Reviewed by Zero Degree on 4/12/2017 02:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.