Loading...

Mbio za mwenge wa uhuru kukimbizwa kwa muda wa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji imeandaa mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda unaohusisha sekta zote za uchumi katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2020; ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati.

Hayo yamesemwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakati akizindua mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dokta Ally Mohamed Shein mkoani Katavi; zenye kauli mbiu inayosema; shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu sera, bunge, vijana, ajira, na walemavu Jenista Mhagama amesema mwenge wa uhuru unadumisha desturi ya kubuni shughuli za maendeleo; huku Waziri wa kazi, uwezeshashi, vijana, wazee, wanawake na watoto kutoka Zanzibar Maudlin Castico akipata nafasi ya kutoa salamu za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Awali Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael muhuga amezungumzia miradi itakayozinduliwa katika mkoa wa Katavi.

Mbio hizo za mwenge wa uhuru kitaifa zitakimbizwa kwa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania bara na visiwani; ambapo zimeanza kukimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya mpanda.
Mbio za mwenge wa uhuru kukimbizwa kwa muda wa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania. Mbio za mwenge wa uhuru kukimbizwa kwa muda wa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania. Reviewed by Zero Degree on 4/02/2017 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.