Loading...

Mlipuko walikumba basi la Dortmund na kupelekea kuahirishwa kwa mechi ya robo fainali UEFA

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imethibitisha kwamba mechi kati ya klabu hiyo na Monaco imeahirishwa.

Hii ni baada ya kutokea kwa mlipuko katika basi lililokuwa linasafirisha wachezaji wa klabu hiyo kwenda uwanjani.

Mechi hiyo ya robofainali katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya sasa itachezwa kesho.

Marc Bartra
Mchezaji wa Dortmund Marc Bartra amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Mashabiki wa Borussia Dortmund
Klabu hiyo imeandika kwenye Twitter kwamba wachezaji wengine wako salama na kwamba hakukuwa na hatari yoyote ndani au karibu na uwanja.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vioo vya madirisha ya basi hilo vimevunjika kutokana na mlipuko huo.

Polisi katika jimbo la North-Rhine Westphalia wamefika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi.

Maafisa wa polisi wamesema kulitokea milipuko mitatu karibu na eneo la basi hilo.

Dortmund kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne katika ligi kuu ya Ujerumani.

Mechi nyingine ya robofainali kati ya Barcelona na Juventus nchini Italia imemalizika kwa Juve kuibuka na ushindi wa goli 3-0, huku magoli ya Juve yakifungwa na Dybala dakika ya 7 na 22 na lamwisho likifungwa na Chiellin dakika ya 55.
Mlipuko walikumba basi la Dortmund na kupelekea kuahirishwa kwa mechi ya robo fainali UEFA Mlipuko walikumba basi la Dortmund na kupelekea kuahirishwa kwa mechi ya robo fainali UEFA Reviewed by Zero Degree on 4/12/2017 12:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.