Loading...

Pluijm kuanza rasmi kibarua Singida United mwezi Juni mwaka huu

KOCHA mpya wa Singida United, Hans van der Pluijm.
KOCHA mpya wa Singida United, Hans van der Pluijm, amesema kuwa ataanza rasmi mazoezi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ifikapo Juni 5 mwaka huu.

Pluijm alisema kuwa tayari ameshaufahamisha uongozi wa klabu hiyo kuanza maandalizi na itakapofika siku hiyo anahitaji kuona wachezaji wote waliosajiliwa wako tayari kuanza kujifua. 

Pluijm alisema kuwa uamuzi wa kuweka kambi ndani au nje ya mkoa wa Singida utajulikana baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

"Programu nyingine kuhusiana na timu siwezi kukueleza kwa sasa, mpaka nitakapofanya mazungumzo na viongozi kwa ajili ya kuweka mambo vizuri, nitakuwa tayari kueleza mikakati yangu baada ya kikao hicho," alisema Pluijm.

Aliongeza kuwa chini yake, anaamini Singida United itakuwa ni moja ya timu zitakazotoa ushindani kwa sababu lengo lake pia ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika kuimarisha kikosi cha Singida United, tayari Pluijm ameshasajili wachezaji wawili wa kigeni na pia anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na wachezaji kadhaa wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwezi ujao.

Mbali na Singida United, timu nyingine ambazo zimepanda daraja na zitacheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ni pamoja na Njombe Mji ya Njombe na Lipuli FC ya Iringa.
Pluijm kuanza rasmi kibarua Singida United mwezi Juni mwaka huu Pluijm kuanza rasmi kibarua Singida United mwezi Juni mwaka huu Reviewed by Zero Degree on 4/19/2017 01:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.