Rais Magufuli ameiagiza TCU kutojihusisha tena na zoezi la udahili wa wanafunzi wa vyuo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza TCU kutojihusisha tena na zoezi la kuwapangia wanafunzi vyuo na badala yake wafanye kazi ya kusimamia viwango vya ufaulu ili kupunguza sintofahamu ya wamiliki wa vyuo binafsi vingine vikiwa havina sifa kuwa karibu na watendaji hao hali inayoweza kuchangia wanafunzi kupangiwa vyuo visivyokuwa chaguo lao.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati akizindua mabweni ishirini ya chuo hicho aliyoahidi miezi nane iliyopita ambayo yatapangishwa kwa wanafunzi kwa gharama ya shilingi mia tano kwa siku tofauti na gharama za mabweni mengine yaliyopo ambayo ni shilingi mia nane na kuongeza kuwa vyuo vingi vyenye ubora vimekuwa vikikosa wanafunzi kutokana na TCU kuwapangia vyuo vingine ambavyo anadhani kuna ujanja ujanja ujanja baina ya watendaji hao na baaadhi ya wamiliki wa vyuo binafsi.
Aidha rais licha ya kupongeza jitihada za kukamilika kwa wakati kwa ujenzi wa majengo hayo amesikitishwa na idadi kubwa ya watumishi hewa,wanafunzi hewa,na mikopo hewa ambayo imekuwa ikiigharimu fedha za walipa kodi huku akibainisha mikakati aliyokwisha ichukua juu ya watumishi wa serikali walighushi vyeti ambao wanafikia elfu tisa nchi nzima.
Awali waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako licha ya kupongeza jitihada za rais Magufuli za kuboresha elimu nchini amewataka wanafunzi kwa manufaa ya umma.
Wakati huo huo rais ametembelea ujenzi wa nyumba za Magomeni na kuweka jiwe la msingi ujenzi utakaogharimu bilioni ishirini kwa nyumba 652 ambapo wakazi 644 watapewa miaka mitanoo ya kuishi bila malipo na baadae watauziwa nyumba hizo.
Rais Magufuli ameiagiza TCU kutojihusisha tena na zoezi la udahili wa wanafunzi wa vyuo
Reviewed by Zero Degree
on
4/18/2017 03:49:00 PM
Rating: