Loading...

Kauli ya Lwakatare baada ya kuteuliwa kuziba nafasi ya Sophia Simba Bungeni

Mchungaji wa kanisa la Assemblies Of God maarufu kama ‘Mlima wa moto’ Dk Getrude Lakwatare, lililopo Mikocheni B, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumkumbuka na kumteua katika nafasi ya ubunge wa Viti Maalumu.

Mama Lwakatare alitoa shukrani hizo wakati wa Ibada ya Pasaka katika kanisa hilo.

“Tunasherehekea kumbukumbu ya kufufuka kwa mwokozi wetu Yesu ambaye alitufia pale msalabani. Pasaka ya mwaka huu ni yangu, Mungu ameniona. “Nina furaha ya mwili na roho kwa sababu Yesu amefufuka na pia Mungu amenirudisha bungeni, Mungu amejibu maombi yetu, tulifunga siku tatu na ile ya mwisho akajibu,” alisema Mchungaji Rwakatare.

Aidha aliongeza kwa kusema ana kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa sababu wapo wanawake wengi ambao angeweza kuwachagua na kuwapa nafasi hiyo huku pia akikushukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumkumbuka.

Machi 11 mwaka huu, Sophia Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alivuliwa uanachama kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama hicho.
Kauli ya Lwakatare baada ya kuteuliwa kuziba nafasi ya Sophia Simba Bungeni Kauli ya Lwakatare baada ya kuteuliwa kuziba nafasi ya Sophia Simba Bungeni Reviewed by Zero Degree on 4/18/2017 03:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.