Loading...

TANZIA: Baba mzazi wa msanii Belle 9 afariki dunia katika ajali ya bodaboda

MSANII wa Bongo Fleva nchini Abednego Damian, ‘Belle9’, amepata pigo baada ya kuondokewa na baba yake mzazi Damian Nyamoga.

Meneja wa Belle9, Jahz Zamba amethibitisha taarifa za hiyo huku akieleza kuwa mzee Damian amefariki dunia kwa kugongwa na bodaboda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro ambako alilikuwa akiishi.

Jahz amfunguka kuwa ni pigo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake kwakuwa mara nyingi amekuwa akidai kuwa baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Staa huyo anayetokea Morogoro amekuwa na mahusiano mazuri na baba yake kama mtu na rafiki yake.

Msiba Upo nyumbani kwa marehemu Morogoro mjini alipokuwa akiishi.
TANZIA: Baba mzazi wa msanii Belle 9 afariki dunia katika ajali ya bodaboda TANZIA: Baba mzazi wa msanii Belle 9 afariki dunia katika ajali ya bodaboda Reviewed by Zero Degree on 4/18/2017 04:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.