Loading...

Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi, mkoani Kilimanjaro

RAIS Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa zinafanyika mkoani Kilimanjaro.

Kwa mwaka huu, pamoja na mambo mengine kilio kikubwa cha vyama vya wafanyakazi ni kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki, alisema Rais Magufuli atazungumza na wafanyakazi katika Sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Aidha, amelishukuru Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) na serikali kwa kuupa heshima ya pekee Mkoa wa Kilimanjaro kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya sherehe za sikukuu hiyo, mwaka huu.

"Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika kilele cha sherehe za wafanyakazi. Pia nashauri wafanyabiashara watumie fursa hii kufanya biashara zako kwa ukarimu na uaminifu mkubwa ili kuwavutia wageni wanaoingia Moshi na watakaoendelea kuja," alisema.

Kwa mujibu wa Sadiki, maadhimisho hayo yameanza kwa kufanyika michezo mbalimbali inayoendelea katika Viwanja vya Ushirika Moshi na washindi wa michezo hiyo watakabidhiwa zawadi zao Aprili 29, mwaka huu.

Aidha, taasisi za afya, mashirika na wadau wa sekta hiyo wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa afya bure.
Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi, mkoani Kilimanjaro Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi, mkoani Kilimanjaro Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 12:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.