Loading...

Kashifa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu inavyozidi kuwaandama wanariadha Kenya

Picha ya mtandao
Chama cha riadha cha kenya kimepata ripoti inayoonyesha kuwa wanariadha wawili wa Kenya wa mbio za masafa marefu, ambao bado hawajatajwa wamepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Mary Keitany aliibuka mshindi katika mbio za London Marathon
Chama hicho kinachelewa kutaja majina ya wanariadha hao kuzuia kuharibu sherehe za kumkaribisha mwanariadha Mary Keitany ambaye alishinda mbio za London Marathon wiki iliyopita na kuvunja rekodi ya dunia.

Jemima Sumgong
Wiki tatu zilizpita mwanariadha mwingine mkenya na mshindi wa zamani wa mbio za London Marathon, Jemima Sumgong, alipigwa marufuku kwa kupatikana kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Baadhi ya wanariadha maarufu wa Kenya wana hofu kuwa sakata hizo huenda zikachafua mafanikio yao na wametaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Kashifa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu inavyozidi kuwaandama wanariadha Kenya Kashifa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu inavyozidi kuwaandama wanariadha Kenya Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 01:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.