Loading...

Simba SC yavutwa mkia mkoani Kagera

Kagera Sugar wameipunguza kasi Simba katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Kipigo walichopata Simba kinawarudisha chini hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakibaki na pointi zao 55 na Yanga sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja huku timu zote zikiwa zimeshacheza mechi 25.

Mshambuliaji wa Kagera Sugar na timu ya taifa Taifa Stars Mbaraka Yusuf alianza kupachika bao la kwanza kwa timu yake dakika ya kipindi cha kwanza kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Simba Daniel Agyei.

Kinda wa Kagera Sugar Christopher Edward akazamisha bao la pili mapema baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuifanya Simba kuwa nyuma kwa magoli 2-0.

Simba ilipata bao lake pekee kupitia kwa Mzamiru Yassin baada ya kutokea piga nikupige kwenye goli la Kagera Sugar.
Simba SC yavutwa mkia mkoani Kagera Simba SC yavutwa mkia mkoani Kagera Reviewed by Zero Degree on 4/03/2017 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.