Loading...

VIDEO: Barca ilivyochakazwa goli 3-0 katika robo fainali ya UEFA dhidi ya Juventus

Barcelona imechabangwa magoli matatu kwa sufuri na Juventus katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Paulo Dybala alifunga magoli mawili katika dakika ya 7 na ya 22. Bao la tatu lilifungwa na Giorgio Chiellini katika dakika ya 55.

Barcelona walicheza kufa na kupona kujaribu kupata japo bao moja la ugenini lakini hawakuweza kufua dafu.

Mchezo mwingine wa robo fainali kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco uliahirishwa baada ya basi ya Dortmund kushambuliwa.

Mchezo wa marudiano ni wiki ijayo.


VIDEO: Barca ilivyochakazwa goli 3-0 katika robo fainali ya UEFA dhidi ya Juventus VIDEO: Barca ilivyochakazwa goli 3-0 katika robo fainali ya UEFA dhidi ya Juventus Reviewed by Zero Degree on 4/12/2017 11:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.