Loading...

VIDEO: Sunderland imeshushwa daraja baada ya kupewa kichapo cha goli 1-0 na Bournemouth

Kipindi cha miaka kumi cha klabu ya Sunderland katika ligi kuu ya Uingereza hatimaye kimekwisha baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Bournemouth nyumbani.

Matokeo hayo pamoja na yale ya sare kati ya Hull City na Southampton yanamaanisha timu hiyo ya David Moyes ina pointi 14 ikiwa imesalia mechi nne.

Joshua King wa Bournemouth alifunga bao la pekee ikiwa imesalia dakika 2 na kuipa ushindi timu yake.

Raia huyo wa Norway pia karibia afunge bao jingine katika dakika ya 20 lakini shambulio lake lilipiga mwamba wa goli na kurudi katika mikono ya kipa Pickford.

Hiyo ni mara ya 23 ya Sunderland kupoteza, hatua inayomaanisha timu hiyo ya Black Cat imeshushwa dajara kutoka ligi kuu ya Uingereza [EPL] kwa mara ya nne.


VIDEO: Sunderland imeshushwa daraja baada ya kupewa kichapo cha goli 1-0 na Bournemouth VIDEO: Sunderland imeshushwa daraja baada ya kupewa kichapo cha goli 1-0 na Bournemouth Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 11:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.