Wakristo wote duniani wanaadhimisha siku ya Ijumaa Kuu leo hii
Ijumaa Kuu huadhimishwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka (kufufuka kwa Yesu), hivyo leo Wakristo dunia wanaadhimisha siku hiyo.
Pasaka huadhimishwa ikiwa ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu, huku viongozi wa dini wakihimiza upendo, msamaha na utu wema.
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba amesema Ijumaa Kuu ni siku muhimu ambayo waumini wa kanisa hilo wanakumbuka fumbo la ukombozi kupitia mateso ya Yesu Kristo.
Amesema Pasaka inaonyesha jinsi Mungu alivyo na upendo uliomuwezesha kumtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo kuteswa kwa kupigwa, kubebeshwa msalaba, kuvalishwa taji la miba na kutobolewa na mkuki hadi kufa ili kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi .
“Hivyo hakuna Pasaka bila Ijumaa Kuu kwa kuwa hapo ndipo tuliona kilele cha upendo wa Mungu kwa wanadamu, sisi,” amesema.

Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2017 09:49:00 AM
Rating: