Loading...

Wamiliki wa vyombo vya usafiri watangaza kusitisha mgomo

Makamu Mwenyekiti wa TABOA, Abdallah Mohammed naye akifafanua Jambo.
UMOJA wa Wamiliki wa Vyombo Vya Usafiri (TABOA) wametangaza kusitisha mgomo wao uliyokuwa ukitarajia kuanza kesho Aprili 4,2017.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TABOA, Mustapha Mwalongo amesema uamuzi huo umefikiwa kufuatiwa kuwepo na mazungumzo baina ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbalawa mapema hii leo na kufikiana mwafaka juu ya walichokuwa wakihitaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe (Katikati) akizungumza na wanahabari.
Aidha amesema serikali kupitia kwa Waziri Mbalawa itarekebisha kanuni na taratibu ikiwemo makosa na adhabu stahiki baina ya madereva na wamiliki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe alisema anashukuru kwa uamuzi huo walioufikia wa kusitisha mgomo wao kwani ungeliweza kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi.
Wamiliki wa vyombo vya usafiri watangaza kusitisha mgomo Wamiliki wa vyombo vya usafiri watangaza kusitisha mgomo Reviewed by Zero Degree on 4/03/2017 10:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.