Loading...

Yanga yaibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam kwenye Ligi kuu ya Vodacom [VPL]

Azam wameshindwa kuendeleza ubabe wao wa kuinyima ushindi Yanga baada ya kukubali kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Tangu mwaka 2014, Yanga ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Azam. Katika kipindi hicho, timu hizo zilikutana mara sita (6) kabla ya leo huku kichezo mitano timu hizo zikiwa zimetoka sare na Azam wakashinda mechi moja.

Yanga imepata ushindi ikiwa inakumbuka kipigo cha goli 4-0 walichokipata toka kwa Azam kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2017 ambacho kilikuwa ni maarufu kwa jina la 4G.

Goli pekee la Yanga kwenye mechi ya leo limefungwa na Obrey Chirwa.

Ushindi wa leo unarudisha matumaini ya Yanga kutetea ubingwa wao baada ya kuejea kileleni kufatia kujizolea pointi tatu na kufikisha pointi 56 pointi moja mbele ya wapinzani wao Simba ambao kesho watakuwa na kibarua cha kuwakabili Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mechi ya leo imeshuhudiwa ikiongeza idadi ya majeruhi kwenye vikosi vya timu zote mbili. Yanga walipata pigo kwa kuondokewa na kiungo wao Justine Zulu ambaye alitolewa uwanjani kwa msaada wa machela na kuwahishwa zahati ya uwanjani kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa upande wao Azam, walimkosa mshambuliaji wao Yahaya Mohamed ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia. Yahaya alisababisha mpira kusimama mara kadhaa ili atibiwe lakini baadae alishindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutoka.
Yanga yaibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam kwenye Ligi kuu ya Vodacom [VPL] Yanga yaibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam kwenye Ligi kuu ya Vodacom [VPL] Reviewed by Zero Degree on 4/01/2017 11:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.